Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi CCM wakielekea katika eneo la kuchangia damu tayari kwa kuchangia kwa hiari
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Geita nao wamejitokeza kuchangia damu kwa hiari.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya Geita katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Geita.
Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM waWilaya Geita mjini wa kimskiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Mbunge wa jimbo la Bukombe na
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa
Mkoani Geita katika Mkutano wa wajumbe wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Geita
ameanza kwa kuwaongoza baadhi ya wajumbe hao kwenda katika eneo la kuchangia
damu kwa hiari ikiwa ni jitihada za kuwanusuru wagonjwa walioko mahospitalini
wenye uhaba wa damu hasa wamama na watoto.
Mwenyekiti huyo aliwaomba wanachama wa Jumuiya ya wazazi CCM kuacha tabia ya kuwachukia viongozi wa vyama vingine vya upinzani kwa kuwa wanatusaidia na kukosowa
tunapokuwa tumeteleza katika utendaji kazi lakini nao wahakikishe wanasema ya kweli
Biteko aliwataka viongozi wa serikali walio chaguliwa nawananchi kupitia CCM kuhakikisha wanafanya kazi walizotumwa na wananchi kwa wakati ili kuleta maendeleo kwa kasi katika taifa na kuweka
pembeni kampeni zisizo na uchaguzi wowote na wasubili 2019 mwaka wa siasa.
Mbunge wa Geita mjini Mhe. Constatine Kanyasu alianza kwa kuwashukuru wanachama kwa kuhakikisha anakuwa mwakilishi wao na kuahidi kuwa hata waangusha na kusema kuwa chama ni mali ya wanachama hivyo wana haki ya kujitathimini mmoja mmoja kama anatosha kuwaongoza na kuwawalisha wenzake na kuongeza kuwa kwa wakati huu ni wakati wa kuwaunga mkono viongozi walioko madarakani kwa pamoja ili kuharakisha maendeleo ya Taifa letu.

Comments
Post a Comment