Shule ya Msingi Ibamba.
Hali halisi ya wanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Ibamba.
Mhe,Doto Mashaka Biteko(Mb) akiwatia moyo wanafunzi wa shule ya msingi Ibamba wanaosomea nje kutokana na ukosefu wa madarasa ya kutosha.
Mhe,Doto Mashaka Biteko(Mb) akiwa na uongozi wa shule ya msingi Ibamba pamoja na watalamu kutoka Wilayani wakijadiliana tayari kwa kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo shuleni hapo.
Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Mkoani Geita Mhe,Doto Mashaka Biteko amekutana na uongozi wa shule ya msingi Ibamba iliyoko Kata ya Uyovu Tarafa
ya Siloka Wilayani Bukombe ikiwa ni hatua ya usimamizi wa fedha zilizotolewa na
Serikali kwa lengo la kujenga vyumba vya madarasa 8 na vyoo 20 vitakavyo
gharimu kiasi cha Tsh. 194,000,000/=.
Katika hatua hiyo Mhe. Biteko aliwasihi
viongozi wa shule wajitahidi kutoa elimu kwa jamii ili wazazi waongeze bidii ya
kuwahudumia watoto wao kwa kuwanunulia vifaa vya shule kwa wakati ili
kushirikiana na serikali inayotoa elimu bure
na kuwasihi wananchi hao kuachana na siasa za kukwamisha maendeleo na kuwaambia wafanye kazi kwa kushirikiana na viongozi wao bila kujali
itikadi zao dini wala ukabila ili kuinua elimu ya shule, wilaya na taifa kwa
ujumla na kusema kuwa wakati wa siasa
sio huu.
Comments
Post a Comment