Mbunge wa Bukombe awataka wananchi kushiriki katika maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko(katikati) na Diwani wa Kata ya Ushirombo Mhe. Lameck Warangi (wa kwanza kushoto) wakiwa wamejumuika kwa pamoja na wanakwaya kwenye mkutano ulioandaliwa na Mbunge huyo.

Katibu Tarafa wa Ushirombo Bw. Lameck Mlugwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Ushirombo









Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kata ya Ushirombo


Hawa ni baadhi ya wananchi wa Kata ya Ushirombo waliouliza maswali katika mkutano wa Mbunge wao

Wananchi baadhi wa Kata ya Ushirombo wakimsikiliza Mbunge wao.

Yaliyotendeka baada ya Mkutano wa Mbunge katika Kata ya Ushirombo.

Bukombe,Mbunge wa jimbo la Bukombe Mkoa wa Geita, Mhe. Doto Mshaka Biteko
amewataka wananchi kuazisha saccos na kuimalisha  vikundi mbalimbali vya
maendeleo ili kunufaika na asilimia tano inayotegwa na halmashauri katika
mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha

Mhe. Biteko aliyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji
cha Businda Kata ya Ushirombo alipokuwa akiwashukuru wananchi kwa
kumchagua kuwa mwakilishi wao Bungeni na kusikiliza kero na maoni  yao.
Alisema vijana na wamama wanapaswa kuanza kuchangamkia fursa ya kuazisha Saccos
na kuunda vikundi mbalimbali vya maendeleo kisha kuanzisha miradi
itakayo wawezesha kupata mikopo toka taasisi mbalimbali za kiserikali
na zisizo za kiserikali.

Biteko alisema yupo tayari kushirikiana na wananchi  hao katika
kujikwamua na wimbi la umasikini kwa kuanza kutafuta tasisi za
kuwaunga mkono jitihada za vijana na wamama watakaojiunga na  vikundi vyenye
miradi  endelevu.

Diwani wa Kata ya Ushirombo Lameck Warangi aliwaomba wananchi kumuunga
mkono Mbunge kwa kuazisha mikakati yakinifu ya kufunga kuku mbuzi na
vijana kuachana na makundi ambayo hayana niya njema katika kuleta maendeleo.
Warangi aliwaomba vijana kubadilika wasikae mitaani badala yake waunde
vikundi na kujishugulisha kufanya kazi za uzarishaji mali ili kuongeza
pato la familia na taifa kwa ujumla.

Mbunge aliwaomba wananchi kuazisha ufungaji wa kuku za kienyeji ili
kulipia ada Sh 10,000 ya mfuko wa maendeleo ya jamii CHF ambayo tayali
itawasaidia kupata matibabu bure kwa mwaka mzima ikiwa yeye mwaka huu
amelipia Sh  milioni 8 Kaya maskini 850 kwa Kata 17 kila Kata ameaza na
Kaya 50.
Pia aliwasisitiza kuwapeleka watoto wao mashuleni kwani elimu inatolewa na serikali bure kwa sasa na kuwataka wananchi hao kushirikiana na serikali kuhakikisha wanatokomeza vipimo vikubwa vinavyowaibia wakulima mazao yao viitwavyo Mozambique walivyonavyo wafanyabiashara wasio waaminifu.    

Comments