Mbunge Doto akiwa Mkoani Geita kikazi atoa msaada kwa watoto wa mitaani

Mbunge wa Jimbo la Bukombe na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM Mkoa wa Geita Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na mmoja wa watoto wa mtaani alipokuwa Mkoani hapo katika ziara ya kikazi.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na mzazi wa Hamad Athuman  ilikujua nini kikwazo kwa mtoto huyo kutokukaa nyumbani na kupata elimu kulingana na umri wake. 
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa katika Ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mseto alikokuwa akisoma awali darasa la tatu kabla ya kuingia mtaani na kuachana na msomo, ikiwa ni hatua ya kumsaidia kumrudisha mtoto huyo aendelee na masomo na kuhakikisha harudi tena kwenye wimbi la watoto wa mtaani.

Comments