Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akifungua michuano ya Ligi ya Doto Cup Fainali ngazi ya Wilaya katika Uwanja wa Kilimahewa uliyoko Mjini Ushirombo.
Moja ya mchezo wa kuvuta Kamba ukiwa ni miongoni wa bonanza katika Ligi hiyo.
Mashabiki wa CCM wakishangilia ushindi wao baada ya bonanza la kuvuta kamba kati ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Vs Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hatimaye CCM kuibuka kidedea na kupewa Zawadi ya Mbuzi na Chadema kupewa Kiasi cha Tsh. elfu ishirini ikiwa ni moja ya mabonanza katika Ligi hiyo ya Doto Cup.
Washindi wa Mchezo wa kuvuta Kamba(WanaCCM) wakiwaonyesha mashabiki Zawadi yao baada ya kukabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Wanachama wa CHADEMA wakiwa jukwaani tayari kwa kupokea zawadi yao baada ya kushiriki mchezo wa kuvuta kamba na kushindwa na WanaCCM na kupata Elfu Ishirini kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Timu ya Kazibizyo Fc nao pia wakipokea zawadi ya mshindi wa Pili Ligi ya Doto Cup kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko.
Timu ya Uyovu Fc wakipokea zawadi ya mshindi wa kwanza Pamoja na Kombe la Ligi ya Doto Cup kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko katika viwanja vya Kilimahewa Mjini Ushirombo.
Huku nafasi ya mshindi wa pili ikishikiliwa
na timu ya Kazibizyo Fc na kufanikiwa
kunyakuwa zawadi ya Jezi pea mbili mpira
mmoja na kiasi cha Tsh Laki mbili na nafasi ya mshindi wa tatu ikikaliwa na
timu ya Namsega Fc baada ya kuichapa
gori 1-0 timu ya Buntubili Fc mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Katika
hatua ya fainali hiyo iliyohudhuria na mamia ya mashabiki Timu ya Uyovu Fc
ilijipatia gori la kwanza dhidi ya Timu ya Kazibizyo Fc dakika 1,dakika ya 5
gori la pili na dakika ya 20 gori la tatu kupitia kwa kiungo mshambuliaji
Deonatus Mkumbulo ‘Ndaki’.
Hadi
dakika ya tisini ya mchezo huo Timu ya Kazibizyo Fc haikupata hata gori la
kufutia chozi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi, Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko amezipongeza timu zote zilizojitokeza
kushiliki ligi hiyo kusema atakuwa
akiandaa Ligi kama hiyo kwa kila mwaka ili kuhakikisha anaendeleza vipaji vya
vijana wanaopatikana ndani ya jimbo la Bukombe waweze kufika mbali na
kuiwakilisha Wilaya ya Bukombe kimchezo.
Comments
Post a Comment