Kamati ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa
Geita imesema wakulima wa Pamba Mkoani hapa hawawajibiki kulipa madeni ya
Pembejeo waliyokopeshwa na UMWAPA, kwa sababu pembejeo hizo hazikuwa na ubora
na zimewasababishia hasara kubwa wakulima wa pamba.
Akizungumza Katibu wa siasa na uenezi CCM Mkoa wa
Geita Bwn. Said Kalidushi amesema hayo
alipokuwa akiongea ya Blogu ya Bukombe sasa kuwa hayo ni maamuzi yaliyofikiwa
kwenye kikao hicho na kwamba wameitaka Serikali kutoa maelekezo hayo haraka
kwenye ngazi za Wilaya ili wakulima wasiibiwe tena.
‘UMWAPA
haitakiwi Mkoa wa Geita kwani wananchi
walitarajiwa kulipwa fidia kutokana na mbegu na madawa yaliyosambazwa na UMWAPA
kukosa ubora kabisa ‘ Alisema Bwn. Kalidushi.
Msimu uliyopita pembejeo zilizo sambazwa kwa
wakulima hazikuwa na ubora kwani mbegu zilizosambazwa hazikuota kwa kiwango cha
kuridhisha na madawa ya kuuwa wadudu hazikuwaua
jambo ambalo limefanya uzalishaji wa zao la Pamba kushuka sana huku wakulima
wakipata hasara kubwa na kuyumba kiuchumi.
Pamoja na kuwepo kwa hali hiyo bado wanunuzi wa
Pamba wakalazimika kudai madeni toka kwa wakulima ambao walisababishiwa hasara
kubwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Bwn. Mashaka
Kasoga,Rashid Mstafa na Samagwa Daniel wame kishukuru sana Chama cha Mapinduzi
(CCM) kwa hatua walizo zichukua dhidi yao ya kuwatetea watu wanyonge kwa
kuwapunguzia adha ya kudaiwa.
Katika hatua nyingine Bwn. Kasoga amewaomba wakulima
wenzake kushirikiana na serikali kwa pamoja ili kuhakikisha kilimo cha Mkataba baina ya
wakulima na mawakala wanao kukopesha pembejeo za kilimo na matokeo yake kupewa pembejeo zisizo na
ubora kabisa wasijitokeze tena.
Comments
Post a Comment