WATU WA NNE WAGUNDULIKA NA SARATANI YA MLANGO WA SHINGO YA KIZAZI-BUKOMBE.




Wito umetolewa kwa wanawake Wilayani Bukombe Mkoani Geita  kujitokeza
kwa hiari kupima saratani ya mlango wa  shingo ya kizazi ili kuepukana
na vifo vya wanawake wengi vinavyotokana na ugonjwa huo kwa kuchelewa
kufikishwa hospitalini.

Rai hiyo imetolewa na kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Dokta
Mahona Kaji wakati wa upimaji wa saratani ya mlango wa  shingo ya
kizazi kwa wanawake hospitalini hapo ambapo amesema 80% ya wanawake
wanaofikishwa katika taasisi ya kansa ocenroad hufikishwa wakiwa
wamechelewa na kuathiri matibabu hali inayopeelekea vifo kwa wanawake
wengi Wilayani Bukombe.

Amesema 50%-60% ya saratani zote kwa wanawake, saratani ya mlango wa
shingo ya kizazi huongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake na kwamba
endapo ikigundulika mapema hufanyiwa matibabu na mgonjwa hupona.

Dr Kaji amesema kutokana na ugonjwa huo kuathiri wanawake wengi wizara
ya afya kwa kushirikiana na shirika la Christian social services
commission ilimeanza mkatati wa uchuguzi wa saratani hiyo kwa wanawake
wenye umri wa kuanzia miaka 15-60 ili kubaini wangonjwa wenye
mabadiliko ya awali  kwa ajiri ya kuanza kupewa matibabu

Hata hivyo kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Wilaya ya Bukombe Dr
Nyamuhanga Range amesema tayari wagonjwa nne wamegundulika wakiwa
wamecheleweshwa kupata matibabu na kupewa rufaa ya kwenda katika
hospitali ya rufaa Bugando iliyopo Mkoani Mwanza ili kupatiwa
matibabu.

Dr Nyamuhanga ametumia nafasi hiyo kutoa kuwashauri kwa wanawake
kujitokeza kwa hiari kupima saratani ya mlango wa shingo ya kizazi
wanawake angalau mara 1 kwa miaka 3 ili kupatiwa matibabu mapema
wakati ilikiwa katika hatua za awali.

Kwa upande wao Naomi stephano na sara matiasi wamewataka wanawake
wenzao kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huo ili kupatiwa
matibabu mapema wakati ugonjwa huo ukiwa katika hatua za awali.

Comments