Wananchi wa Kijiji cha Nampalahara wakimpokea Mbunge wao Mhe. Doto Mashaka Biteko na Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe. Nikas Mayala
Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe. Safari Nikas Mayala akizungumza na wananchi wa Kata hiyo
Picha ya baadhi ya waliyouliza maswali kwenye mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko katika Kijiji cha Namparahara Kata ya Busonzo.
Wananchi wa Kata ya Busonzo Wilayani ya Bukombe wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwasaidia kuihimiza serikali ili iwaletee miradi ya visima virefu kwani adha ya huduma ya maji ni kubwa mno.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao
bi Matha Petro na Bw Emanuel Philip wamesema kuwa
wamekuwa wakiteseka sana kupata maji hasa wakati wa kiangazi kwani
visima walivyonanyo ni vya muda mfupi (wakati wa masika)na vingine ni visima
vivilivyochimbwa kina kifupi na kuwa na uchache wa maji.
Katika hatua
nyingine bw Emanuel Philip amemuomba Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto
Mashaka Biteko kuwasaidia kupata Kituo cha Afya na Shule kwani watoto wao
wamekuwa wakienda mbali kupata elimu na kutokufika kwa wakati na wengine hata
kukata tamaa ya kuendelea na masomo.
Pia Diwani wa Kata
ya Busonzo Mhe. Safari Nikas Mayala amewataka wananchi hao kuachana na maswala
ya kisiasa na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mbunge wao Mhe. Doto Mashaka
Biteko ili kuendelea kufanya maendeleo ya pamoja kwa maslahi ya Kata, Wilaya
na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mbunge
wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko ameahidi kushirikiana na serikali katika
ujenzi wa Barabara ya Uyovu- Bwanga iliyokuwa imekwama kwa mda wa miaka mitatu
bila mafanikio hivyo kuwashauri wananchi kuendelea kujishughulisha na miradi ya
maendeleo kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.
Katika hatua
nyingine Diwani wa Kata ya Busonzo Mhe. Safari Nikas Mayala ametoa shilingi laki tano na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka
Biteko ametoa mifuko hamsini ya sementi ikiwa ni juhudi za kuwaunga mkono wananchi
katika ujenzi wa shule ya msingi Gengeni iliyoko Kijiji cha Namparahara.
Comments
Post a Comment