Diwani wa Kata ya Lyambamgongo Mhe. Boniphace Shitobelo akizungumza na wananchi wa Kata yake
Mtumishi wa Mungu akifanya maombi kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Lyambamgongo katika mkutano wa hadhara.
Mbunge wa Jimbo la
Bukombe Mkoani Geita Mhe,Doto Mashaka Biteko amefanya ziara katika Kijiji cha
Lyambamgongo, Kata ya Lyambamgongo, Tarafa ya Bukombe Wilayani Bukombe na
kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji hicho.
Katika mkutano huo Mhe,
Doto Biteko(Mb) amewashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mwakilishi wao na kuahidi
kutowaangusha na kusema atawasilisha Bungeni yale watakayo sema wananchi na sio
mawazo yake hivyo wamuunge mkono na kumuombea.
Aidha katika mkutano huo
wananchi waliorodhesha changamoto zao ikiwa ni miundo mbinu duni ya
barabara,ukosefu wa kituo cha afya,ukosefu wa malisho ya mifugo yao na kucheleweshewa pembejeo za kilimo hali inayowakwamisha katika uzalishaji bidhaa zinazotokana na kilimo cha mazao na
kusababisha uchumi wao kuyumba.
Aidha Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Biteko
amewaomba wananchi wajitahidi kuwahudumia watoto wao kwa kuwanunulia vifaa vya
shule kwa wakati ili kushirikiana na serikali inayotoa elimu bure na kuwasihi wananchi hao kuachana na siasa za
kukwamisha maendeleo na kuwaambia
wafanye kazi kwa kushirikiana na
viongozi wao bila kujali itikadi zao dini wala ukabila kwani Tanzania ni moja
na wakati wa siasa sio huu.
Comments
Post a Comment