
Baada ya
Bunge la Tanzania kupitisha marekebisho ya sheria ya kodi ya ongezeko la
thamani ‘VAT’ ya mwaka 2014 kuanzia July 01 2016 kwenye huduma za
kifedha kwa kurekebisha kifungu cha 13 cha jedwali la msamaha wa kodi.
Mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji kuhusu marekebisho hayo ya sheria. Leo July 01 2016 Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania ‘TRA’, Alphayo Kidata amezungumza na waandishi wa habari na kusema
>>>kuna
taarifa ambazo si za kweli zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii
kuwa VAT itatozwa kwanye amana ya mwenye fedha kwenye benki. Hii siyo
kweli, ukweli ni kuwa kiasi cha VAT kitakachotozwa ni asilimia 18 ya
kiasi cha gharama ya huduma iliyotolewa na benki au taasisi yoyote ya
fedha.
Kidata ameeleza mfano huu………>>>Ada
ya hudum ya benki ambayo mteja ametozwa ni sh 1000 kodi ya ongezeko la
thamani itakayotozwa kwenye kiasi hiki ni sh 152.50 tu na benki kubaki
na sh 847.50 kiwango hicho cha sh 152.50 ndicho kitakachorejeshwa
serikalini na benki au taasisi ya fedha baada ya kupunguza kodi ya
ongezeko la thamani iliyolipwa kwenye manunuzi ambayo yamefanywa na
benki au taasisi ya fedha husika.
TRA
imezitaka benki na taasisi za fedha zilizoamua kwa makusudi kutoa
taarifa zisizosahihi kwa umma kuacha mara moja vinginevyo hatua kali
zitachukuliwa, aidha imeziagiza benki na taasisi zinazohusika
kurekebisha mara moja taarifa walizokwishazisambaza ili zibebe maudhui
sahihi ya marekebisho ya sheria hii.
Comments
Post a Comment