TIMU YA NARUSUNGUTI YA IBUKA KIDEDEA KATIKA LIGI YA DOTO CUP

Wachezaji wakiwa uwanjani


Picha ya kamati ya usimamizi wa michezo kati ya Busonzo 



Picha ya anae husika na huduma ya kwanza







Wachezaji wakiwa na mashabiki kwa pamoja wakisubiri hatua ya utoaji wa zawadi


Afisa Mtendaji wa Kata ya Busonzo Bw Shitwala Lukuba akitoa zawadi kwa mshindi.

 
Timu ya Narusunguti Fc iliyopo  Kata ya Busonzo Wilayani Bukombe Mkoani Geita jana imejinyakulia  zawadi ya kiasi cha shilingi elfu hamisini na mpira moja baada ya kuichapa gori 1-0 Timu ya Mtunduni Fc katika hatua ya fainali ya vijiji vinavyounda Kata ya Busonzo katika  ligi ya Doto Cup  iliyohitimisha hapo jana katika uwanja wa Namparahara.
Mechi hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki katika uwanja wa Namparahara Timu ya Narusunguti ilichapa gori 1 Timu ya Mtunduni Fc dakika ya 42  kupitia kwa kiungo mshambuliaji Nyorobi Benard.
Hadi dakika tisini ya mchezo huo Timu ya Mtunduni fc haikupata hata gori la kufutia chozi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi,  Afisa Mtendaji wa Kata ya Busonzo Bw Shitwala Lukuba amezipongeza timu zote zilizojitokeza kushiliki ligi hiyo  iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa lengo la kuendeleza vipaji vya vijana wanaopatikana ndani ya jimbo la Bukombe. 
Katika finali hiyo Timu ya Narusunguti Fc iliibuka na zawadi ya  mshindi wa kwanza kwa kupata mpira 1 pamoja na   kiasi cha shilingi elfu hamsini huku Timu ya Mtunduni Fc ikipata   zawadi ya mshindi wa pili  kwa kupata mpira moja.
Kwa upande wake kocha wa timu ya Mtunduni Fc Bw Burugu Yeyema ameshukuru kwa timu yake kupata nafasi ya pili katika ligi hiyo na kuwataka wachezaji wa timu yake kutokata tamaaa kutokana na kusindwa kufikia  malengo waliyokuwa wamejiwekea ya  kushika nafasi ya kwanza na kunyakuwa zawadi hiyo nono na kuwasihi  wachezaji wake kuendelea kufanya mazoezi kwa bidii ili kuendeleza vipaji vyao.
Nae kocha wa timu ya wa timu ya Narusunguti Bw Yohana Tomasi amewashukuru wachezaji wake kwa ushindi walioupata na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwa bidii ili  kufika  hatua ya finali ngazi ya wilaya.
Aidha baadhi ya mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo Joseph Makoba na Mariamu Mitinje wamekishukuru chama cha mpira wilayani hapa  kwa kusimamia vizuri ligi ya doto cup ngazi ya vijiji na kuwataka kuendelea kuboresha ligi hiyo katika ngazi ya kata, tarafa na wilaya  kwa kuweka waamuzi wenye sifa zinazokubalika ili  kutenda haki katika ngazi zote.



Comments