Sikukuu ya Eid El Fitri yaazimishwa Bukombe

Shekhe wa msikiti wa  wamasijid Nuru Ushirombo Ostadhi Abudman Yasini akitoa mawaidha katika viwanja vya Bulangwa wakati wa  Eid El Fitri



Kaimu shekhe wa Wilaya  Ally Jumapili  akizungumza na waumini wa wa dini ya kiislamu wakati wa ibada ya  Eid El Fitri


 Waumini wakijiandaa kwa kutoa swadaka

Wamama wa kiislam wakisikiliza mawaidha katika viwanja vya Bulangwa wakati ibada ya Eid El Fitri

Picha ya pamoja ya viongozi wa dhehebu la kiislamu Wilayani Bukombe baada ya ibada ya  Eid El Fitri



Waumini wa dini ya kiislamu Wilayani Bukombe Mkoani Geita, wamehimizwa kuendelea kudumu katika imani ya kiislamu wakati wote na kusimamia mafundisho waliyoyapata wakati wa mwenzi mtukufu wa ramadhani.
Akizungumza katika ibada ya Eid El Fitri Shekhe wa Msikiti wa  Masijid Nuru Ushirombo Ostadhi Abudman Yasini amewataka waiislamu kudumu katika imani hasa katika mafundisho waliyoyapata katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani na kuendelea kujitenga na mambo yasiyompendeza mwenyezi  mungu wakati wote
Amewataka waislamu kuendeleza upendo na kuwa wakarimu kama wanavyoelekezwa na viongozi wao kwa kuwasidia wasiojiweza katika kupata mahitaji muhimu katika maisha yao.
Kwa upande wake Kaimu Shekhe wa Wilaya  Ally Jumapili  amewataka waumini wa dini hiyo kuendelea kufanya kazi zao kwa uaminifu na uadilifu na bila dhuluma kwa kuwa dini inakataza mdhuluma kwa  mwiislamu  na kupenda kufanya kazi za kuwaingizia kipato kwa njia halali  ili kuendelea kujenga uchumi wa  nchi ya Tanzania na kuacha matendo yasiyo mpendeza mwenyezi mungu.

Comments