Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Msangila kabla ya kuelekea mkutanoni
Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Msangila baada ya kufika mkutanoni hapo wakiwa wamebeba mabango
Picha ya baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Msangila wakimsikiliza Mbunge wao
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe,Doto Mashaka
Biteko amefanya ziara katika Kijiji cha Msangila, Kata ya Runzewe Magharibi,
Tarafa ya Siloka Wilayani Bukombe na kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji
hicho.
Katika mkutano huo Mhe, Doto Biteko(Mb) amewashukuru wananchi
kwa kumchagua na kukubali kujitokeza katika mkutano huo ili kujadiliana
mustakabali wa maendeleo na changamoto za eneo hilo.
Aidha katika mkutano huo wananchi waliorodhesha changamoto
zao ikiwa ni ukosefu wa pembejeo,miundo mbinu duni ya barabara,ukosefu wa kituo
cha afya,ukosefu wa malisho ya mifugo yao,kutafutiwa soko la mazao yao hasa
udaga na kuomba kuimarishiwa ulinzi na usalama ndani ya kata hiyo
Katika hatua nyingine wanafunzi wa Shule ya msingi Msangila
iliyoko Kata hiyo wameandama hadi kwenye
mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe, Doto Mashaka Biteko
wakiomba kutatuliwa changamoto
zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa vifaa
ya michezo, hali inayowafanya kushindwa kushiliki michezo shuleni .
Wakizungumza na blog ya Bukombe sasa wameiomba serikali kuwajengea visima vya maji, , vyoo, walimu wa
kutosha kutokana na uhaba mkubwa wa walimu walionao na madawati hali
inayowafanya wanafunzi zaidi ya 120 kukaa chini .
Wanafunzi hao waliokuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa
Aidha Mbunge wa Jimbo
la Bukombe Mhe. Doto Biteko amesema atashirikiana na wananchi hao kwa karibu
kuhakikisha wanamaliza changamoto zao na kama si kuzipunguza na kuahidi
kuwapatia wanafunzi hao vifaa vya michezo ikiwemo seti ya jezi za wasichana na wavulana,
mipira na nyavu kwa ajiri ya kushiriki michezo wawapo shuleni.
Comments
Post a Comment