Abiria wakishauliana la kufanya baada kutelekezwa
Hali halisi ya abiria hao baada ya safari kukwama
Askari Polisi akiwasikliza abiria hao
Basi ya Kampuni ya Falcon yenye namba za usajiri T415 DCJ inayo fanya safari zake Bukomba - Dar Es Salaam imetelekeza abiria wake 60 katika stendi ya mabasi mjini Ushirombo Wilayani Bukombe Mkoani Geita, Dereva, kondakta na tingo kuwakimbia watejawao bila ya taarifa.
Wakizungumuza kwa nyakati tofauti abiria hao
Hames Issa mwenye tiketi yenye namba 145873 amesema safari ya kutoka Dar Es
Salaam stendi Ubungo iliaza jana Julai
17 majira ya saa 12:00 asubuhi lakini kufika Gairo walitumia masaa tisa Dodoma,
Singida walifika saa 8:00 usiku hali ambayo siyo ya kawaida.
Issa amesema Julai 18 majira ya saa 5:00
asubuhi tuliigia Ushirombo wakati wakiwa ushirombo Kondakta wa bas hilo
aliwaomba kuwa wavumilivu gari tangu
jana linatatizo lakini cha kushangaza hadi saa 8:00 mchana hatuoni hata mmoja
wamekimbia kusiko julikana
.
Abiria mwenjiristi wa kanisa la (SDA) Sevet
dey Advetntista wasabato Siaberth Terugwa mwenye tiketi namba 145202 amesema
amelipa nauri harali Sh 60,000 kutoka Dar Es Salaam hadi Bukoba alikuwa anaenda
kwenye msiba akisubiliwa nyumbani kwa ajiri ya mazishi ya dada yake katika kijiji cha Kasharu kata ya
Kasharu Wilaya ya Bukoba vijiji Mkoani
Kagera.
Terugwa alitaja changamoto aliyoipata baada
ya kukimbiwa na Dereva,Kondakta na taniboi
kutojulikana waliko kwenda nakwamba kibaya zaidi hata fika kwenye
mazishi ya ndugu yake na tayali amesha luhusu mazishi yaendele kutokana na
changamoto hiyo aliomba serikali kuingiria kati ili gari hilo liweze
kuwafikisha wanako kwenda lakini kutokana kutoelewana vizuriabilia
wameingiwa hofu na wasiwasi yakutokufika
salama Bukoba hivyo serikali iliagalie na isimamie warudishiwe nauri zao na
watafute basi jingine la kuwafikisha Bukoba.
Meneja wa usafirishaji wa kampuni ya Falcon yenye
tin: 104-443-249 Rovikoki Maro amesema
amepata taarifa za basi kuhalibika kutoka kwa abiria lakini anajalibu kutafuta
mawasiliano ya Dereva na Kodakta hawapatikani lakini tagu jana wakiwa Morogoro
wamekaribia Dodoma lilitokea tatizo la mfumo wa gia lakini aliwasiliana nao
na tatizo lili patiwa ufumbuzi na safari iliendelea.
Maro amesema kuhalibika kwa basi Ushirombo
Wilayani Bukombe hajapata taarifa na kwamba anafanya mawasiliano na Dereva na
Kondakta bila mafanikio ili kama kunatatizo kubwa afanye mawasiliano ya kuagiza
Basi Jingine la kampuni yao ya Falcon zilizopo Geita ili ichukue abilia waendele na
safari ya kwenda Bukoba.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Mponjoli
Mwabulambo simu yake ya mkononi ilipokelewa na walinzi wake na kusema kuwa yuko
kwenye kikao lakini awali polisi Wilaya ya Bukombe wamefika stendi na
kuthibitisha changamoto za abilia na kwamba Wanawatafuta Dereva na Kodakta wa
basi hilo ili kuhakikisha wanaendelea na safari yao.
Comments
Post a Comment