Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga(mwenye suti katikati) na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya pamoja na Daktari wa Kituo cha Afya Uyovu (mwenye koti jeupe)wakielekea kwenye mradi wa ujenzi wodi ya wazazi itakayofunguliwa na mwenge wa uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita Josephat Maganga
ameanza ziara yake ya kwanza katika Tarafa ya Siloka Wilayani Bukombe kwa
kutembelea miradi mbalimbali ya
maendeleo itakayozinduliwa na kuwekewa
jiwe la msingi julai 31 mwaka huu.
Bw Maganga ametembelea katika Kituo cha Afya cha Uyovu
kukagua mradi wa ujenzi wa wodi ya wazazi na chumba cha upasuaji (Theater)unaofadhiliwa
na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na idadi ya watu(UNFPA) na ugawaji
wa vyandaruwa vyenye dawa, mradi wa ujezi wa Barabara ya Uyovu, Kabagole na
Nakayenze, Mradi wa ujenzi wa soko la mazao ya biashara Namonge, Vyumba vya
Madarasa na Nyumba za walimu (six in one) katika shule ya sekondari Namonge na
ujenzi wa josho la kuogeshea ng’ombe katika Kijiji cha Msonga.
Picha ya miradi iliyokaguliwa wakati wa ziara ya Mkuu wa Wilaya Bukombe
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya wakikagua Mradi wa ujenzi wa soko la mazao ya biashara Namonge
Nyumba za walimu (six in one) katika shule ya sekondari Namonge
Katika ziara hiyo mkuu wa Wilaya Josephat Maganga ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya
ulinzi na usalama kumtambulisha kwa wakazi wa maeneo ya Tarafa ya Siloka na
kujua vipaumbele vyao katika kusukuma maendeleo ya Wilaya ya Bukombe.
Moja ya vibaumbele vya wananchi hao kwa Mkuu wa Wilaya Josephat Maganga ni kuendelea kujenga
umoja wa wananchi, kuboresha sekta ya kilimo cha mazao ya biashara na chakula
kwa kutoa pembejeo za kilimo kwa wakati, kuboresha sekta ya elimu kwa kwa
kuhimiza serikali kujenga vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, madawati na
mabweni kwa wanafunzi wa kutwa, na kuboresha sekta ya afya hasa kujenga vituo
vya afya katika kila kata ili kuokoa vifo visivyo vya razima kwa kutembea
mwendo mrefu kutafuta matibabu.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bukombe amesema atahakikisha anatoa ushirikiano wa kutosha
kwa wananchi hao hasa katika maswala ya kuiweka wilaya hiyo kuwa salama na
kuhimiza maendeleo kwa wananchi na kuwataka viongozi walio katika ngazi za
Tarafa, Kata ,Vijiji na Vitongoji kutenda haki na kusimamia ukweli kwa maslahi ya Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Comments
Post a Comment