Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake Mkoani Geita 2016

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Generali Mstaafu Salim Mstafa Kijuu na Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Ezekiel Kyunga wakikabidhiana Mwenge wa Uhuru tayari kwa kuanza mbio zake  katika Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Generali Ezekiel Kyunga akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Josephat Maganga tayari kwa kuweka jiwe la msingi na kuifungua miradi ya maendeleo iliyoko katika Wilaya hiyo ya Bukombe.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akiwa ameubeba Mwenge wa Uhuru baada kukabidhiwa na Viongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Wilayani Bukombe.


Picha ya baadhi ya vikundi vya sanaa vilivyoshiriki kuupokea Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita.

 Picha ya baadhi ya Wananchi wa Kjiji cha Kanembwa Kata ya Uyovu Wilayani Bukombe pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Geita waliojitokeza kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika kiwanja cha shule ya msingi Kanembwa



Comments