Mechi ya Ufunguzi wa Ligi ya Doto Cup ngazi ya Tarafa



Viongozi wa Chama cha Mpira  Wilayani Bukombe(BUFA),katibu wa Mbunge Jimbo la Bukombe na baadhi ya mashabiki wakishuhudia mechi ya ufunguzi wa Ligi ya Doto Cup ngazi ya Tarafa 
 
Timu ya Ituga fc imeichapa gori 1-0 timu ya Lyambamgongo fc katika ufunguzi wa Ligi ya Doto Cup ngazi ya Tarafa iliyofanyika katika uwanja wa Kijiji cha Bukombe Tarafa ya Bukombe  Wilayani Bukombe mkoani Geita.

Mechi hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki,timu ya Ituga fc ilijipatia gori dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Jofrey Maiga, hadi dakika 90 timu ya Lyambamgongo haikupata hata gori la kufutia chozi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ligi ya Doto Cup ngazi ya Tarafa katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe ndugu Benjamini Mgeta amesema Ligi hiyo ni kwa ajili ya kukuza na kuinua vipaji ya vijana Wilyani hapa na kuwataka wachezaji wanaoshiriki Ligi kufanya mazoezi zaidi kabla ya kushiriki mechi ili kujiweka sawa katika kunyakuwa zawadi ya mshindi wa kwanza ngazi ya Wilaya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Mpira Wilayani hapa bw Peter Bomani amesema atahakikisha haki inatendeka kwa kila timu inayoshiriki Ligi hiyo na kwamba atasimamia vyema   sheria na kanuni za mpira wa miguu ili kupata timu bora ya Wilaya kupitia Ligi ya Doto Cup.

Comments