Baadhi ya Wafugaji wa Wilaya ya Bukombe waliojitokeza kushiriki katika kikao cha ndani cha Wafugaji katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Runzewe
Wafugaji wa Wilayani Bukombe Mkoani Geita, wamehimizwa
kuendelea kudumu katika umoja na ushirikiano wakati wote na kusimamia ukweli
ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima katika jamii inayowazunguka.
Akizungumza katika kikao hicho Diwani wa Kata ya Busonzo na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Mhe. Nikas Mayala Safari amesema
kila hatua inagharama zake na kuwaomba wafugaji wasivunjike moyo katika suala
zima la ufugaji kwani ipo siku jambo la malisho ya mifugo yao litapatiwa
mwafaka wake.
Pia mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Kanda ya Ziwa(CHAWAKAZI) Bw. Juvenari Mlashani
amewataka wafugaji wote kushiriki kikamilifu katika huduma za kijamii bila
kujali itikadi, dini wala ukabila ili kujiletea maendeleo kwa haraka na
kuimarisha uchumi wao na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka
Biteko ameanza kwa kuwapa pole wafugaji
kwa misukosuko yote iliyojitokeza na kuwataka wafugaji kutokata tamaa ya
kuendelea kufuga na kuwasihi kuzidi kushikamana
kwa pamoja wao kwa wao na kushikiana na serikali ili kuharakisha mafanikio na
kuwaomba wawe tayari kubadilika kwenda kwenye ufugaji wa kisasa kilingana
mifugo kuzidi kuongezeka na ikiwa eneo ni lilelile .
Comments
Post a Comment