Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko na Diwani wa Kata ya Katome Mhe. Paul Mhangwa wakibadilishana mawazo kabla ya mkutano kuanza.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa kata ya Igulwa.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita Mhe,Doto Mashaka
Biteko amefanya ziara katika Kata mbili za Katome na Igulwa Wilayani Bukombe na kufanya mikutano ya
hadhara katika Kata hizo.
Katika mikutano hiyo Mhe, Doto Biteko(Mb) amewashukuru
wananchi kwa kumchagua kuwa Mbunge wao na kuwasihi wananchi hao kuachana na
itikadi za vyama dini na ukabila kwa wakati huu na badala yake kila mwananchi
ashirikiane na viongozi walioko madarakani kwa pamoja
kuleta maendeleo katika Wilaya yao ya Bukombe.
Aidha katika mikutano hiyo wananchi waliorodhesha changamoto
zao huku wakianzia Kata ya Katome kwa kusema changamoto zao ni kutozwa pesa
kwenye huduma za afya za mama na mtoto,ukosefu wa visima virefu,pembejeo
kutokufika kwa wakati na unyonywaji wa
wakulima kwa wafanya biashara wa mazao
kwa kuwapimia kwenye kipimo kisicho sahihi(Mozambiki)
katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Bugama
Katika upande wa Kata ya Igulwa wamesema changamoto zao ni
ukosefu wa miundo mbinu ya barabara,huduma ya maji safi,kukosa choo cha
wanafunzi shuleni,kituo cha afya,wingi wa wanafunzi shuleni na waalimu ni
wachache,vifo vya wachimbaji wadogo kwa kukosa vifaa vya kisasa vya kuchimbia
madini na migogoro ya wafugaji na wakulima kugombania maeneo ya kuchungia
Wananchi wa Kata ya Igulwa wakimsikiliza Doto Mashaka Biteko (Mb)
katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Buntubili
Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano hiyo amasema kuwa atahakikisha
anashirikiana na serikali ili umeme vijijini uwenee kwa wingi kwa kuviingiza
vijiji hivyo kwenye mpango wa umeme vijijini REA na kuongeza mawasiliano ya
barabara zinazounganisha maeneo mbalimbali hususani kijiji na kijiji, kata na
kata na hata wilaya na wilaya kwa kuziingiza kwenye mfuko wa TANROAD baadhi ya
barabara hizo na kuwaomba wananchi hao kujitoa kwa dhati kwenye shughuli zozote
za maendeleo.
Comments
Post a Comment