Maandalizi ya kupunguza changamoto ya madawati Bukombe

Mwenyekiti wa Kikundi cha Runzewe Development Group(R.D.G) na Igunanilo Group Dr. Baraka Charles Kulwa akiangalia umaliziaji wa madawati. 

Picha ya baadhi ya madawati yaliyotengenezwa

Baada ya upungufu wa madawati Wilayani Bukombe Mkoani Geita, vikundi vya Runzewe Development Group(R.D.G) pamoja na Igunanilo Group vimeamua kutengeneza madawati 60 na zoezi la utengenezaji wa madawati  bado linaendelea, uongozi wa Runzewe Development Group (R.D.G) na Igunalilo Group natarajia kukabidhi madawati yote kwenye halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ili mgao wa madawati hayo ufanyike katika shule zinazo kabiliwa na upungufu wa madawati wilayani hapa ili wanafunzi wanaokaa chini waondokane na changamoto hiyo.
Akizungumza Mwenyekiti wa vikundi hivyo Dr. Baraka Charles Kulwa amesema anamshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa hamasa alizozifanya wakati akizunguka jimboni kwake kwenda kuhamasisha maendeleo na kuviomba vikundi na taasisi vilivyo na uwezo kujitokeza kuchangia madawati ili kupunguza changamoto zilizoko kwenye shule za msingi na sekondari  wilayani hapa .

Comments