Mbunge wa jimbo la Bukombe Mhe Doto Biteko(aliyesimama) akizungumza na Halmashauri ya CCM ya Wilaya ya Bukombe.
Moja ya mumbe akichangia mada
Taarifa ya utendaji wa Mbunge wa Jimbo la Bukombe ameitoa kama ifuatavyo
OFISI YA MBUNGE JIMBO LA BUKOMBE
TAARIFA
YA UTENDAJI KWA HALMASHAURI KUU YA CCM YA WILAYA, KATIKA KIPINDI CHA NOV 2015-
JUNE,2016
10/7/2016.
1.Utangulizi
Mheshimiwa
Mwenyekiti, kama unavyofahamu ofisi yako ilisimamia vema uchaguzi
wa mwaka 2015. Juhudi zako na ofisi yako ziliniwezesha kuchaguliwa kuwa mbunge
wa jimbo la Bukombe.
Naomba nikushukuru sana wewe na watendaji wote wa ofisi
yako kwa ushirikiano, miongozo na maelekezo mbalimbali mliyonipatia wakati wote
wa kampeni. Maelekezo yenu ndiyo yaliyofanya tushinde vizuri katika uchaguzi
huo.
Hata hivyo naomba niombe radhi ikiwa kwa namna moja au
nyingine sikufanya vizuri katika kuzingatia maelekezo ya ofisi yako.
Mheshimiwa
Mwenyekiti, baada ya uchaguzi kinachofuata ni kazi.
Kazi ya kutekeleza ahadi zote zilizoahidiwa wakati wa kampeni. Aidha ni wakati
wa kuisimamia serikali ili itekeleze vyema ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kiwango
cha kupimika. Kutokana na ukweli huo, mimi kama mbunge nalazimika kutoa taarifa
kwa chama na nimejiwekea utaratibu wa kutoa taarifa kila baada ya miezi sita.
2.
Mhutasari wa kazi zilizofanyika kwa kipindi cha novemba 2015 –Juni,2016
Tukio
|
Yaliyofanyika
|
Matokeo
|
1.
Uundaji wa ofisi ya mbunge
|
·
Katibu wa CCM kata ya Uyovu aliteuliwa kuwa katibu wa
Mbunge
·
Ofisi ya mbunge kwenye chama ilifunguliwa
|
|
Uundaji wa akamati ya mfuko wa jimbo
|
|
|
2.
Ziara
a)
Mikutano ya Hadhara na ya ndani ya CCM
|
·
Mbunge ametembelea jumla ya kata 16 kati 17
·
Ahadi kadhaa zilitolewa na mbunge
|
·
Hoja mbali mbali ziliibuliwa na jumla ya maswali zaidi
ya 900 yaliulizwa na kufafanuliwa kwenye mikutano hiyo.
·
Ahadi mbalimbali zimeshatekelezwa na nyingine
zitakamilishwa mwezi huu.( Angalia
kiambatisho na2)
·
Kero mbalimbali zilipatiwa ufumbuzi mf. Uwepo wa ofisi
ya TANESCO Bukombe na uongezwaji wa nguzo za umeme kwenye mradi wa
electricity iv.
·
Ukarabati wa barabara ya Katoro Ushirombo ushakamilika.
·
Jumla ya madai ya walimu 208 yalishughulikiwa na
kurekebishwa kwenye Lawson utumishi
·
Ukaguzi ulifanyika kujua kama kweli fedha 10,000,000/
zilizodaiwa kuibiwa kwenye akaunti ya kijiji Ng’anzo.
·
Vipimo vya Mozambique vimefutwa na maelekezo ya vipimo
vya mazao ya nafaka yametolewa.
·
Miradi ya MIVARF imeanza kutekelezwa uyovu na Namonge
·
Mwekezaji Ng’anzo aliahidi kukamilisha ujenzi wa
nyumba za walimu na kifusi kilichokua kinaingia kwenye nyumba za watu kimerekebishwa.
|
b).
Kutembelea taasisi
|
·
Kituo cha afya uyovu kilitembelewa
·
Walimu wa kata ya Runzewe Magharibi walitembelewa
·
Hospitali ya wilaya ilitembelewa
·
Kituo cha polisi Uyovu kilitembelewa
·
Runzewe sekondari
|
Kero
mbalimbali zilitolewa na watumishi wa taasisi hizo na majibu yaltolewa
|
3.
Maafa/Majanga
|
·
Kitongoji cha Idoselo nyumba 40 zilichomwa moto na
maofisa wa maliasili
·
Familia iliyopata matatizo ya kufariki mama na watoto
kwa kula chakula kilichodhaniwa kuwa na sumu
|
·
Wahanga walitembelewa na mikutano miwili ilifanyika na
misaada ya chakula na maturubai vilitolewa.
·
Wafiwa walitembelewa na kupewa mkono wa pole
|
4.
Mialiko kwa mawaziri
|
Mialiko
hii ni kutokana na uwepo wa changamoto zilizohitaji utatuzi kutoka serikali
kuu.
|
·
Mawaziri jumla ya ziara 6 wa sekta mbalimbali waheshimiwa,
(Mwigulu Nchemba, Eg. Ramo Makani, Dr. Medard Kalemani, Prof. Jumanne
Maghembe na Hamad Masauni)
walifika na kusaidia kutatua changamoto
hizo.
|
5.
Mikutano
|
Mikutano
mbalimbali ya kazi ilihudhuriwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa, Taifa na nje
ya nchi.
|
·
Mbunge alihusika katika kutoa maamuzi na aidha
kuwakilisha bunge kwenye mikutano nje ya nchi.
|
6.
Harambee na machangizo mbalimbali
|
Utoaji
wa michango ulifanyika kwenye makanisa mbalimbali na tasisi nyingine
|
Uimarishaji
wa mahusiano na kukuza imani ya wanachi kwa viongozi wao.
|
7.
Michezo
|
Vifaa
mbalimbali vya michezo vimegawiwa kwa vijana ikiwemo jezi na Mipira.
Ligi
ya jimbo imeanza
|
Michezo
imeendelea kufanyika
Ligi
inawendelea
|
3.
Kuitambulisha wilaya ya Bukombe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ili
maendeleo yafike mahali popote lazima kwanza mahali hapo pajulikane. Duniani
sehemu kubwa ya fedha za makampuni au taasisi 40% ya mapato yao huenda katika
kujitangaza. Na Bukombe inahitaji kujitangaza ndani na nje ya nchi ili
kuwavutia wawekezaji katika kushiriki uchumi wetu.
Ili kutekeleza hili blogu maalumu ya Bukombe imeanzishwa
iitwayo BUKOMBE SASA na tumeiweka kwenye PLAY STORE ya simu zote. Mtu anaweza
kupata taarifa yoyote kupita blogu.
Mheshimiwa
mwenyekiti, naomba sote tuitembelee blogu hii kwa anuani
ya bukombesasa.blogspot.com
aidha unaweza kuipakua
kwenye playstore ya simu yako ikiwa una smart phone.
4.
Mafanikio
Mheshimiwa
Mwenyekiti,
Katika kipindi hiki cha miezi 6 ya mwanzo yapo mafanikio
kadhaa ambayo kwa kweli ofisi yako pia imeshiriki kufanya yatokee.
·
Wananchi kuwa na matarajio chanya na Mbunge
wao
·
Seikali ya awamu ya tano imekuwa nyepesi
sana tunapo hitaji msaada wake mfano mmeona
kila tunapoarika mawaziri wanakuja kwa haraka kutusikiliza na kutatua
changamoto zetu kwa kiasi kikubwa.
·
Misaada na huduma mbali mbali kwa uchache zimetolewa
kwa wananchi kama inavyoonyeshwa kwenye kiamabtisho na 2.
·
Kwa kushirikiana na mbunge wa Mbongwe tunashawishi
kupandisha daraja barabara itokayo
ushirombo – Katome- Mbongwe- Bukoli
·
Aidha kwa kushirikiana na Mbunge wa Chato
tunashawishi kufungua barabara ya kutokea Kakoyoyo kwenda Bwanga kupitia
Nyikonga.
·
Tumefanikiwa kupata madawati ya 400 toka
Tamisemi ambayo yamegawanywa kwenye shule 10.
·
Tumekubaliwa na wizara ya mambo ya ndani
kupata gari moja kwaajili ya kituo cha polisi uyovu. Aidha tunatarajia kufungua
kituo kidogo cha polisi Namonge
·
Miradi ya MIVARF hatimaye imeanza
kutekelezwa kwa kujenga soko la kisasa huko Namonge na barabara ya kabagole.
·
Wanafuzi na walimu wa uyovu sekondari
walipewa zawadi kwa kufanya vizuri kitaaluma.
·
Kuingiza vijiji vyote kwenye mradi wa umeme
vijijini
·
Kuanzishwa kwa ofisi ndogo za TANESCO
Bukombe.
·
Kuanzisha ligi ya jimbo kama ilivyoahidiwa
wakati wa kamapeni.
·
Tumeingiza kwenye miradi ya maji mwaka huu
wa fedha vijiji 10
5.
Changamoto
Mheshimiwa
mwenyekiti, naomba nilete changamoto chache zinazoikabili ofisi ya
mbunge. Changamoto hizi tunaweza kwa pamoja kuzipunguza kama siyo kuzimaliza
kabisa. Zifuatazo ni changamoto chache:
·
Upatikanaji wa fedha za miradi kwa wakati
imekua ngumu kidogo. Mfano mwaka tuanomalizia ni 26% tu ya fedha za miradi
zilipelekwa
·
Jimbo la bukombe limeaminishwa na wanasiasa
kuwa wananchi wanapaswa kufanyiwa kila kitu na serikali jambo ambalo si sahihi.
·
Uwepo wa zahanati chache na vituo vya afya
vichache vimefanya utoaji wa huduma za afya kuwa ngumu kwa watoa huduma
6. Hitimisho
Mheshimiwa Mwenyekiti,
naomba nihitimishe tena kwa kukushukuru wewe na kamati yako ya siasa na
halmashauri kuu ya wilaya ya ccm kwa kukubali kunitengea muda huu ili kupokea
taarifa yangu. Taarifa ni mhtasari tu wa mambo mengi yaliyofanyika kwa kipindi
cha miezi 6.
Ninaomba
sasa taarifa hii ipokelewe na kujadiliwa.
Imetayarishwa
na:
Doto
Biteko (MB)
Mbunge
jimbo la Bukombe
NAOMBA
KUWASILISHA
Kiambatisho
Mgawanyo wa fedha za mfuko wa Jimbo
1.
Madawati 10,000,000/
2.
Uendeshaji 2,000,000/
3.
CHF 8,500,000/
4.
Choo
Kilimahewa 1,700,000/
5.
Kidete
s/m 5,000,000/
6.
Bugama
S/M 5,000,000/
7.
Wazee 500,000/
8.
Ushirombo
S/M 3,000,000/
9.
Kapwani
S/M 1,500,000/
10. Msonga Sekondari 3,000,000/
11. Bulega Sekondari 3,000,000/
12. Bulangwa S/M 2,000,000/
13. Choo Nyamakunkwa 2,000,000/
14. Buntambala S/M 3,000,000/
15. Choo Busonzo S/M 3,000,000/
Comments
Post a Comment