TIMU YA ITUGA FC YAPATA USHINDI KATIKA LIGI YA DOTO CUP.

Kiungo mshambuliaji wa Timu ya Ituga FC,Gilad Lukiko" akiichambua ngome ya Timu Nasihukulu, katika mchezo uliopigwa jioni hii, ikiwa ni mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Kombe la Doto Cup ngazi ya Kata uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Bukombe

Wachezaji wa Ituga fc na mashabiki wao wakishangilia ushindi wao dhidi ya Nasihukulu fc



Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa ligi ya Doto Cup akitoa maelekezo kuhusu zawadi za washindi


 




Timu ya Ituga Fc iliyopo  Kata ya Bukombe Wilayani Bukombe Mkoani Geita leo imejichukulia  zawadi ya kiasi cha shilingi elfu hamisini na mpira moja baada ya kuifunga gori 2-0 Timu ya Nasihukulu Fc katika hatua ya fainali ya vijiji vinavyounda Kata ya Bukombe katika  ligi ya Doto Cup  iliyohitimisha hii leo katika uwanja wa Shule ya msingi Bukombe.

Mechi hiyo iliyohudhuliwa na mamia ya mashabiki pamoja na Mbunge wao Mhe. Doto Mashaka Biteko katika uwanja wa Shule ya msingi Bukombe Timu ya Ituga fc iliifunga gori la kwanza Timu ya Nasihukulu Fc dakika ya 22 kipindi cha pili  kupitia kwa kiungo mshambuliaji Gilad Lukiko na kuongezwa tena dakika ya 40 kipitia kwa mchezaji huyohuyo

Hadi dakika tisini ya mchezo huo Timu ya Nasihukulu fc haikupata hata gori la kufutia chozi pamoja na jitihada za golikipa kuingia uwanjani kutafuta goli .


Akizungumza Mbunge wao Mhe Doto Mashaka Biteko mara baada ya mchezo kuisha amezipongeza timu zote zilizojitokeza kushiliki ligi hiyo  na kuwasihi walioshinda kuongeaza juhudu kwenye ngazi zinazofuata iliwaweze kufanya vizuri na hatimaye kupata ushindi nakwa upande wa walioshindwa amewaeleza wasikate tamaa kuendeleza  vipaji vyao  
 ili kuendeleza vipaji vyao.


 


Comments