Timu ya Bulama fc wakiwa na moja wa kiongozi wao kabla ya kianza mchezo
Picha ya pamoja ya timu ya Ikuzi fc
Wachezaji wa Timu ya Ikuzi fc wakifanya mazoezi kabla ya mchezo kuanza
Kamati ya usimamizi wa Ligi ya Doto Cup Kata ya Runzewe Mashariki wakiwakagua wachezaji kabla ya kuanza kwa mchezo kwenye kiwanja cha Msonga
Kiongozi wa Timu ya Bulama fc ambae ni mshindi wa pili katika fainali hiyo akionyosha zawadi kwa mashabiki wake
Picha ya pamoja ya viongozi wa kamati ya Ligi ya Doto Cup na Timu ya Ikuzi fc iliyochukua ubingwa wakionyesha zawadi kwa mashabiki wao
Picha ya pamoja kwa timu zote zilizoshiriki fainali wakiwa na Kamati ya Usimamizi wa Ligi ya Doto Cup Kata ya Runzewe Mashariki na washabiki wao
Jana timu ya Ikuzi fc imeichapa gori 2-0 timu ya Bulama fc
katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Doto Cup ngazi ya kata uliofanyika katika uwanja wa Msonga uliopo Kata ya Runzewe Mashariki Wilayani Bukombe Mkoani Geita
Mchezo huo uliokuwa wa kushindania zawadi ya kiasi cha
shilingi elfu 50 na mpira mmoja kwa mshindi wa kwanza
na mshindi wa pili akipata mpira mmoja timu ya Ikuzi fc ilifanikiwa kunyakua
zawadi hiyo nono baada ya kuichapa gori 2-0 timu ya Bulama fc
Gori la kwanza la Timu ya Ikuzi fc imetiwa nyavuni na
mchezaji Vitina Kabili dakika ya 18 na
gori la pili na la tatu yamefungwa na kiungo mshambuliaji Yosamu Julius dakika ya 25 katika kipindi
cha kwanza.
Hadi dakika tisini ya mchezo huo Timu ya Bulama fc
haikupata hata gori la kufutia chozi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi, Afisa Mtendaji wa Kata ya Runzewe Mashariki Bwana Nestory amezipongeza timu zote zilizojitokeza kushiliki ligi hiyo iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe
Mhe. Doto Mashaka Biteko kwa lengo la kuendeleza vipaji vya vijana wanaopatikana ndani
ya jimbo la Bukombe .
Comments
Post a Comment