WAISLAM WA BUKOMBE- GEITA WASHIRIKI FTARI YA PAMOJA ILIOANDALIWA NA MBUNGE

Waumini wa dhehebu la kiislam wakipewa maelekezo na mmoja wa kiongozi wao

Kaimu Shekhe wa Wilaya ya Bukombe Ali Jumapili (kulia) wakiwa na baadhi ya viongozi wenzake




Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM Wilaya ya Bukombe)Bwn Zacharia Bwire akiwa katikati ,kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Bukombe Bwn Michael Bundala na Kulia ni Katibu wa CCM Kata ya Igulwa Bwn Mstafa wakipata ftari ya pamoja.



Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko (alieshika kikombe) akiwa na baadhi ya waumini pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukombe Mhe. Safari Mayala (mwenye suti nyeusi) kwenye ftari ya pamoja.

 Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Aman Mwinegoha(katikati),kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Bukombe Michael Bundala na kushoto ni mmoja wa waumini wa kiislam walioshiriki jambo hilo tukufu la kufuturu.




Waumini wa dini ya kiislamu Wilayani Bukombe mkoani Geita, wameiomba
serikali  kumaliza kero ya  mifugo ya  Nguruwe inayoendelea kuzaga
mitaani hasa wakati huu wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Wameyasema hayo jana katika ftari ya pamoja iliyoandaliwa na mbunge wa
jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko ambapo wamesema kuwa wanyama hao
wamekuwa kero kutokana na  kuachiwa ovyo mitaani hali inayosababisha
baadhi yao kuingia kwenye nyumba za waislamu na kukaribia  nyumba za
ibada kutokana na Ufugaji horela usiozingatia sheria za kufuga
wanyama.

Kwa upande wake Kaimu   Shekhe wa Wilaya  Ally Jumapili  amesema  kuwa
kwa muumini wa dini ya kisilamu ni kikwanzo kikubwa  kukutana na mnyama
nguruwe  wakati akielekea msiktini hasa wakati huu wa mwezi mtukufu wa
ramadhani kwa kufikilia kuitendea jambo baya mifugo hiyo na
kusababisha swaumu yao isikubalike.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Amani Mwenegoha  amesema kutokana mifugo hiyo kuwa kero kwa  waisilamu na jamii nzima kwa ujumla
ametoa siku tatu  kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe James Ihunyo kuanzia Juni 23 hadi Juni 27 kuhakikisha wanatoa Elimu kwa wafugaji wa mifungo hiyo ili waache tabia ya kuiachia mifugo hiyo  ovyo.

Mbunge wa jimbo la Bukombe Dotto Biteko wakati akitoa shukrani kwa
waumini wa dini hiyo ya kiislamu kukubali kuhudhuria jambo hilo tukufu
amewaomba waislamu kuendelea kuiombea amani nchi ya Tanzania  kutoana na serikali ya awamu ya tano kuelekea katika uchumi wa kati na kuwataka wananchi kubadilika ili kuendana ka kasi ya sasa  ili kujiletea maendeleo.


Comments