Rais Magufuli Aanza Kubanwa....Atakiwa Kutangaza Rasmi Tarehe za Kukamilisha Hatua za Kuandika Katiba



RAIS John Magufuli ametakiwa kutangaza rasmi tarehe na namna ya kurejea kwenye mchakato wa kuandika Katiba Mpya ili kukamilisha hatua zilizobaki, anaandika Pendo Omary. 

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) katika mkutano maalum na waandishi wa habari.
 

Deusi Kibamba, Mwenyekiti wa JUKATA amesema, tathimini jumala ya taasisi hiyo mebaini kwamba, mchakato umeshidwa kujenga muafaka wa kitaifa unaohitajika kama za la mchakato wa katiba na hivyo kupelekea katiba inayopendfekezwa kuwa na kiwango duni cha maridhiano ya kitaifa.
 

“Kwa hapa tulipo, mchakato wa Katiba unahitaji nguvu ya ziada ili uanze mapema katika mwaka wa fedha unaoanza wiki mbili zijazo kwa sababu mchakato haukuahirishwa kisheria kwa mtindo wa tangazo la serikali kabala ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 

“Pia, zaidi ya kugusiwa na Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa Bunge mwishoni mwa mwaka 2015, haijaonekana nia wala dalili za serikali kutaka kurejesha mchakato wa katiba mpya. Ndio maana JUKATA tunaungana na Rais Mstaafu Benjamini Mkapa katika hoja kuwa mjadala wa kitaifa unahitajika sasa,” amesema Kibamba na kuongeza;


“Bila Katiba Mpya yenye misingi imara ya utawala bora utumbuaji majipu na ‘hapa kazi tu’ inaweza kuwa kauli mbiu zisizoeleweka kwa Watanzania kwa kukosekana misingi imara ya kikatiba na sheria wa utekelezaji wake.
 

Kibamba amesema, namna utumbuaji majipu unavyofanyika wakati mwingine unaonekana kuvunja heshima, utu na faragha ya binadamu pamoja na misingi mikuu ya haki za binadamu kwa mujibu wa Katiba.
 

Aidha, JUKATA limeitaka serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka bungeni miswada ya kurekebisha sheria zinazosimamia mchakato wa wa katiba kwa ajili ya kuzihuisha katika tarehe zake zote zilizopitwa na wakati.

  
Hatua hiyo inatokana na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 na ile ya Kura ya Maoni ya mwaka 2013 kupitwa na wakati na haziwezi kutumika tena bila marekebisho, bunge la bajeti kuelekea kumalizika bila miswada wa marekebisho ya sheria hizo kupelekwa bungeni na hakuna bajeti iliyotengwa katika suala la katiba kwa mwaka wa fedha 2016/2017

Comments