Mhe. Doto Mashaka Biteko (Mb)(wakatikati),kushoto ni Diwani wa Kata ya Katente Mhe. Bahati Kayagila na kulia ni Kaimu Afisa Madini wa Mkoa wa Geita bwn. Fabian Mshai wakiwa na wananchi wa Kata ya Katente kwenye bicon aliyoweka mwekezaji.
Mchimbaji mdogo akifanya utafiti wa madini
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi wa Kata ya Ketente.
Picha ya baadhi wananchi wa Kata ya Katente wakimsikiliza Mbunge wao Doto Mashaka Biteko.
Wananchi wa Kata ya Katente wakimsindikiza mbunge wao Mhe Doto Mashaka Biteko(katikati) baada ya mkutano nao katika Kata hiyo.
Wananchi
wa Kijiji cha Katente Kata ya Katente Wilayani Bukombe mkoani Geita wameiomba serikali kumaliza mgogoro baina ya
wachimbaji wadogo wa madini na mwekezaji
katika eneo hilo kwa kuwapatia suluhu.
Wakizungumza
katika mkutano wa Kijiji hicho na mbunge
wa Jimbo la Bukombe mh. Doto Biteko
wakati wakitafuta suluuu ya mgogoro
wamesema kuwa muwekezaji alivamia
maeneo yao kwa madai kuwa ana kutaka kuwekeza katika maeneo yao bila makubalino
na wamiliki wa maeneo husika.
wamesema kuwa maeneo hayo wameyamiliki kwa muda mrefu
na kwa kuyatumia katika shughuli za
uchimbaji mdogo, kilimo,ufugaji na makazi.
Kwa upande
wake mbunge wa Jimbo la Bukombe Mh. Doto Biteko amesema kuwa serikali ya awamu
ya tano haipo kwa ajili ya kuwakandamiza wananchi wa hali ya chiini hivyo
lazima muwekezaji yeyote afuate sheria
za uwekezaji.
Katika hatua
nyingine Mhe. Biteko amemuunga mkono mkuu wa Wilaya ya Bukombe Aman Mwinegoha kwa kitendo cha kusimamisha zoezi la mwekezaji huyo hadi atakapofuata
sheria zote za uwekezaji wa madini ili isiwepo migogoro tena.
Aidha kaimu afisa madini mkoa wa geita bw
Fabian mshai amewataka wamiliki wa maeneo kuendeleza shughuli zao za kila siku
ikiwemo kilimo, ufungaji na makazi hadi
hapo watakapo maliza migogoro yao baina ya mwekezaji na wamiliki wa maeneo
good job mheshimiwa
ReplyDelete