ZIARA YA BAADHI YA MADIWANI WA BUKOMBE MJINI DODOMA

 Msafara wa Mhe. Doto Mashaka Biteko(Mb) na Baadhi ya Madiwani pamoja na Wafugaji wa Bukombe Mjini Dodoma.



Picha ya Waheshimiwa Madiwani wa Bukombe na Wafugaji wakiwa nyumbani kwa Waziri Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Nchemba


Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe waliwasili Dodoma kwa ziara ya siku mbili kuanzia Mei 25 hadi 26/2016 katika Mji Mkuu wa Tanzania (Dodoma).
Ikiwa malengo ya ziara yao mara baada ya kuwasili mjini hapo walisema lengo kuu la ziara yao ni kwenda kujionea na kujifunza miradi mbalimbali ya maendeleo, kujionea shughuli za Bunge na kujadiliana na Mbunge wao Mhe. Doto Mashaka Biteko jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali  ili kuwepo ufugaji bora na kilimo cha kisasa zaidi na kuondoa migogoro baina ya wafugaji,wahifadhi na wakulima.    

Comments