Rais Magufuli ateua mwingine Ukuu wa Wilaya
Baadhi ya
wilaya ziliachwa wazi na Wakuu wa Wilaya baada ya kuteuliwa katika
nafasi zingine za uongozi, April 18 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania John Pombe Magufuli amemteua Hamphrey Polepole kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.
Polepole anachukua
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Kamishna
Msadizi mwandamizi wa polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Uteuzi wa Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016.
Humphrey Polepole
Comments
Post a Comment