TATIZO LA MADAWATI BUKOMBE

Wapendwa tuna tatizo kubwa la madawati kwenye wilaya yetu ya Bukombe.
Mchanganuo ufuatao unaonyesha hali halisi ya mahitaji:



Elimu Awali
                       Mahitaji    8,268
                       Yaliyopo      288
                        Upungufu  8,080

Shule za msingi
                        Mahitaji   16,307
                        Yaliyopo    7,498
                         Upungufu  8,809

Shule za Sekondari
                        Mahitaji   8,312
                        Yaliyopo   5,225
                        Upungufu 3,123
Jumla ya Mahitaji yote ni Madawati 20,012
(Source: Bukombe DC)

Tumepata msaada madawati 400 na tumeyagawanya kwa kuangalia shule msingi zenye hali mbaya zaidi. Mgawanyo huo ni kama ifuatavyo:
  • Ibamba S/M (Kata ya Uyovu)                        Madawati 100
  • Nampalahala S/M  (Kata ya Busozo)             Madawati   50
  • Azimio S/M (Kata ya Bulangwa)                   Madawati   50
  • Namonge S/M  (Kata ya Namonge)               Madawati 100
  • Nyikonga S/M  (Kata ya Bulega)                   Madawati   50
  • Msangila S/M  (Kata ya R/Magharibi)           Madawati   50
Aidha Halmashauri imeanza mkakati wa kutengeneza madawati zaidi.
Kwa wapenda Bukombe waliopo Bukombe na Nje ya Bukombe Tunawaomba kama wadau wa elimu pia kujitokeza kusadia kumaliza changamoto hii.
ELIMU KWA WATOTO WETU NDIYO URITHI WA KWELI

Comments