Sentensi za CCM kuhusu uteuzi wa msemaji mpya wa chama aliyechukua nafasi ya Waziri Nape

Ni March 20, 2016 ambapo chama cha mapinduzi kilifanya mkutano na waandishi wa habari na kumtangaza msemaji mpya wa chama cha mapindizi baada ya waziri Nape kuteuliwa kufanya kazi za uwaziri kulitumikia taifa.


Akizungumza na waandishi wa habari katibu mkuu wa chama hicho, ndugu Abdulrahman Kinana  alisema…‘Bw.Christopher Sendeka yeye sasa ndio atakuwa msemaji wa chama cha mapinduzi kwasababu gani, kwasababu katibu mwenezi wa chama chetu ndugu Nape aliteuliwa kuwa waziri wa Serikali na Waziri wa habari  utaratibu wa chama chetu nafikiri ni busara mtendaji wa chama anapoteuliwa kuwa waziri basi atajishughulisha na kazi yake ya uwaziri lakini kwasababu katibu mwenezi ameteuliwa na halmashauri kuu ya taifa, uteuzi wake unateguliwa tu na halmashauri kuu kama alivyoteuliwa na halmashauri ya kitaifa’ – Kinana
MSEMAJIIII
Kushoto ni Christopher Ole Sendeka akizungumza baada ya kuteuliwa.Kulia ni katibu wa NEC, itikadi wa uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni waziri wa Habari , Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo
‘Kwahiyo hakuna mwenye mamlaka wa kutengua uteuzi wake isipokuwa halmashauri ya kitaifa kwahiyo atabaki kwa jina kuwa mwenezi wa chama chetu mpaka hapo halmashauri kuu itakapokaa kutengua nafasi hiyo aliyonayo ya mwenezi, lakini tungependa kazi ya kuisemea chama cha mapinduzi kiendelee kwahiyo tumemteua bwana Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji wa chama chetu’ – Kinana 
chanzo ; Edwini TZA

Comments