RAISI MAGUFULI ATEUWA WAKURUGENZI WA TAASISI YA TBC ,NSSF NA RAHCO

Tanzania's President elect John Pombe Magufuli addresses members of the ruling Chama Cha Mapinduzi Party (CCM) at the party's sub-head office on Lumumba road in Dar es Salaam, October 30, 2015. Tanzania's ruling party candidate, John Magufuli, was declared winner on Thursday of a presidential election, after the national electoral body dismissed opposition complaints about the process and a demand for a recount. The election has been the most hotly contested race in the more than half a century of rule by the Chama Cha Mapinduzi Party, which fielded Magufuli, 56, a minister for public works. REUTERS/Sadi SaidRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Profesa Godius KahyararaMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Profesa Godius Kahyarara (kushoto).liyobaMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.
KWANZA, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Uteuzi huu umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.
Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
PILI, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Dkt. Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu.
TATU, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO).
Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Uteuzi wa watendaji wote watatu umeanza mara moja
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
19 Machi, 2016.

Comments