KUFUNGWA KWA SOKO LA SAMAKI - USHIROMBO

Ushirombo; Wauzaji wa samaki mjini Ushirombo wamefungiwa soko lao kulingana na kukithili kwa uchafu sokoni hapo.



Akizungumza Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao (Bwana Paul) alisema, uchafu huo wa samaki waliotumbuliwa,kuparuliwa na kukaangwa kumesababisha uchafu mwingi utakao leta maradhi katika soko hilo. Hivyo waliamliwa na Maafisa wa Afya na Mkuu wa Wilaya kufunga soko hilo kwa shughuli za uparuaji na ukaangaji na kubaki huduma ya uuzaji wa samaki wabichi, baadaye kuwapeleka nyumbani kwa ajili ya ukaangaji na kuwarudisha sokoni wakiwa tayari wamesha kaangwa ili kupunguza wingi wa uchafu katika soko jambo ambalo ni changamoto kwa wafanyabiashara hao.
                                      
                                                  Hali ya Jalala la zamani 
                                                 Hali ya Jalala jipya

   











Ombi la wafanyabiashara hao kwa Serikali ni kuboreshewa huduma ya maji, meza za kisasa na mifereji ya kutilili majitaka. 

Comments