MABINGWA WA MIKOA BUKOMBE COMBINE SC ZATOSHANA 0-0 MABAO FC MCHEZO WA KIRAFIKI


 Katika mchezo huo  timu zote zimetoka sare ya 0-0 mchezo huo ulihusisha mabingwa wa mkoa wa Geita daraja la tatu Bukombe Combine SC na mabingwa mkoa wa Shinyanga Mabao fc. 

Timu hizi mbili ni miongoni mwa timu za mabingwa wa mikoa nchini kwa lengo la kucheza ligi hiyo ngazi ya kanda kila moja ikiwania kupanda daraja la pili.

Kwa upande wake  kocha wa timu ya Bukombe combine sc James Kishimba alisema mchezo ulikuwa mzuri na vijana wamecheza vizuri licha ya kuwa changomoto zilikuwepo chache kutokana na uwanja haukuwa mzuri. 

Mkurungezi wa mabao fc akizungimzia timu yake alisema namshukuru Mungu mchezo umemalizika salama hakuna majeruhi kwa timu zote kwayo ni Jambo jema na mchezo ulikuwa mzuri sana ivo tutarajie mengi na mazuri kuelekea ligi ya mabingwa wa mikoa ngazi ya kanda. 


Afisa habari wa timu ya Bukombe Combine SC Zena Seleman aliwaomba mashabiki pamoja na wadau wamichezo kuendelea kuwaunga mkono timu ya Bukombe Combine sc kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji wao

,,Huu ni mwanzo tu sisi Kama timu tumejipanga vizuri kuelekea katika mechi zijazo za mabingwa wa mikoa vijana wanamazoezi yakutosha hakuna kitakacho haribika tunawaahidi ushindi kwetu ni lazima hivyo mkae mkao wa kula", alisema selemani. 


Comments