STAR BOYS FC YAWASHUSHIA KICHAPO USHIROMBO STAR GOLI 3-2




Timu ya Star boys fc imewashushia kichapo cha magori 3-2 timu ya Ushirombo star ya Ntegele kwenye ligi ya Doto Cup 2019 uwanja wa michezo Kata ya Bulangwa Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita.

Wafugaji wa magori timu ya Star boys fc Daud Emmanuel dakika ya 15 goli la pili pia Daud Emmanuel dakika ya 38 goli la tatu limefungwa na Richard Kandolo dakika ya 63.

 Aliyefuga goli la timu ya Ushirombo star Pasi Kuya dakika ya 28 goli la pili lilifungwa na Mfaume Mtimbe dakika ya 75  na kufikia mwisho wa kushiriki ligi ya Doto Cup 2019 huku wenzao Star boys fc wakijipanga kukutana na timu nyingine.
 
 Mchezeshaji wa mechi hiyo Magela Kilosa alisema kunawachezaji wawili wa timu ya Star boys fc wamemaliza mchezo wanakadi za njano katika michezo yao wabadilike watakuja kupewa kadi nyekundu huku timu ya Ushirombo star wakitoka na kadi moja ya njano.

Mshabiki wa timu ya Ushirombo star Joel Simon akilaumu wachezaji kuwa wamefungwa kutokana na kuachia nafasi ya maadui wao upenyo huku wakijuwa ligi hii ukipigwa ndo umetoka hadi mwakani.

Msimamizi wa ligi ya Doto Cup 2010 Kata ya Bulangwa Marco Nsolo alisema lengo la mdhamini wa Ligi hiyo Mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Mashaka Biteko ni kuwaunganisha vijana kwenye michezo na kutambua kuwa michezo ni ajira.

Comments