
Mwenyekiti huyo wa CCM alieleza hilo jana kwenye hotuba yake wakati wa
mapokezi ya ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyowasili nchini
jana mchana Januari 11, 2019 kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius
Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
''Dkt. Bashiru amekuwa muwazi, huwa namuangalia kwenye hotuba zake saa
nyingine nasema kumbe mimi nafuu bwana kuliko huyu jamaa'', alisema.
Rais alieleza kuwa Katibu wake huyo amekuwa akikemea ufisadi ambao
ulikuwa ukishamili siku hadi siku lakini sasa yeye anapingana nao
hadharani bila kujali.
Magufuli amewataka viongozi wote wa chama na Serikali kuendelea
kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja ili kusaidia maendeleo na siku moja
Tanzania itakuwa kama Ulaya.
Comments
Post a Comment