Emmanul
Macron ambaye hakujulikana katika siasa miaka na kabla ya miezi kumi na
tatu ya wa uchaguzi wa urais hakua na chama chochote, alichaguliwa
Jumapili hii Mei 7 kuwa rais wa nane wa awamu ya tano akiwa na miaka
39.Emmanuel Macron aliibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Marine Le Pen
katika duru ya pili kwa 66.06% ya kura.
Katika
taarifa yake, Emmanuel Macron alisema kwamba Ufaransa imefanikiwa
kufungua ukurasa mpya katika historia yake na kwamba alikuwa na ndoto ya
kuwa mpiga mbiu wa nchi hiyo kwa kugunduliwa upya kwa matumaini na
imani.Mshndi huyo wa nafasi ya urais ametoa hotuba yale ya kwanza akiwa
ni raisi mteule. Emmanuel Macron, amenukuliwa akisema kwamba
atahakikiksha anafanya kila linalowezekana kulipa fadhila ya uaminifu wa
wafaransa waliompa.
Macron
pia alitoa shukrani kwa wapiga kura ambao hawakumpigia kura akisema
wametekeleza haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi waliyemtaka ambapo
amesema licha ya yote hayo bado anawaona ni raia wa Ufaransa na
wanastahili kusikilizwa.
"Wafaransa
wenzangu, mlioko ndani na nje ya ufaransa, baada ya vita ya muda mrefu
vya kidemokrasia , na kuchagua kuweka imani yenu juu yangu. Ningependa
kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa heshima kubwa".
Macron
alisema jukumu lililoko mbele yake ni kuhakikisha analinda maslahi ya
taifa la Ufaransa kwenye umoja wa Ulaya na kwamba kama alivyoahidi
wakati wa kampeni anataka kuona Ulaya mpya chini ya uongozi wake.
Facebook Blogger Plugin by
Comments
Post a Comment