KAIMU KAMISHNA WA MAADILI AWAAPISHA KIAPO CHA UADILIFU WAKUU WA WILAYA WATEULE WA WILAYA ZA MTWARA NA UBUNGO.


 Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri Yahaya Kipacha akiwaapisha Wakuu wa Wilaya wateule Mhe. Kisare M. Makori (Ubungo) na Mhe. Evod Mmanda Herman (Mtwara) kiapo cha Uadilifu katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri Yahaya Kipacha leo amewaapisha Kiapo cha Uadilifu Wakuu wa Wilaya Wateule Mhe. Evod Mmanda Herman (Mtwara) na Mhe Kisare M. Makori (Ubungo) katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Picha zote  na Ally Mataula – Afisa Habari – Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri Yahaya Kipacha akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mteule Mhe. Evod Mmanda Herman mara baada ya tukio la kiapo cha Uadilifu lililofanyika  katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri Yahaya Kipacha akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Evod Mmanda Herman mara baada ya tukio la kiapo cha Uadilifu lililofanyika  katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mteule Mhe. Evod Mmanda Herman kulia na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe Kisare M. Makori wakisaini Hati zao za Uadilifu mara baada ya kula kiapo cha Uadilifu mbele ya Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri Yahaya Kipacha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamishna wa Maadili Bw. Waziri Yahaya Kipacha kushoto aliyesimama akizungumza na Wakuu wa Wilaya Wateule Mhe. Evod Mmanda Herman (Mtwara) wa kwanza kulia aliyekaa na Mhe. Kisare M. Makori (Ubungo) wa pili kulia aliyekaa mara baada ya tukio la kiapo cha Uadilifu lililofanyika  katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.

Comments